Muda mfupi baada ya kuwasili jijini Mbeya asubuhi ya leo kikosi chetu kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Sokoine kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons.
Kikosi kimewasili jijini hapa leo Oktoba 19, saa mbili asubuhi na saa nne kikaelekea Uwanja wa Sokoine kwa ajili ya mazoezi ya kuendelea na maandalizi ya mchezo.
Makipa Beno Kakolanya na Ally Salum wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Sokine, Mbeya
Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ameuchukulia mchezo dhidi ya Prisons kwa umakini mkubwa kutokana na uimara wa wapinzani na aina ya mpira wa nguvu wanaocheza.
Baada ya kambi ya muda mfupi hapa jijini Mbeya kikosi kitaelekea mjini Sumbawanga kwa ajili ya mchezo wetu utakaopigwa Uwanja wa Nelson Mandela Alhamisi Oktoba 22.
Kiungo Francis Kahata akifanya mazoezi katika Uwanja wa Sokine, Mbeya kujiweka fiti kuwavaa Tanzania Prisons mechi itakayochezwa Sumbawanga
Kiungo Jonas Mkude akifanya mazoezi na wenzake katika Uwanja wa Sokine, Mbeya