Habari za Michezo kote Ulimwenguni

Powered by Blogger.

Baada ya tizi la Zambia,Simba kuifuta Prisons Sumbawanga

 

Kikosi chetu kitaelekea mjini Sumbawanga leo Jumanne Oktoba 20 jioni, tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Alhamisi katika Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.
Beki wa kati Joash Onyango na straika Miraj Athumani wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Nakonde nchini Zambia

Timu iliondoka asubuhi jijini Mbeya kuelekea nchini Zambia ambapo tumefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Nakonde kujiweka sawa. Kesho timu itafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Nelson Mandela kabla ya keshokutwa jioni kushuka dimbani kuivaa Prisons.

Popular Posts