Sports News

Habari za Michezo kote Ulimwenguni

Powered by Blogger.

BERNARD MORRISON AACHWA BONGO SIMBA IKIKWEA PIPA




KIUNGO wa Simba, Bernard Morrison ameachwa kwenye msafara wa wachezaji uliokwea pipa leo Desemba 18 kuwafuata wapinzani wao FC Platinum ya Zimbabwe.



Nyota huyo ambaye alisajiliwa kwa mbwembwe akitokea Klabu ya Yanga kwa dili la miaka miwili amekuwa hana nafasi ndani ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck.

Mbali na Morrison nyota mwingine ambaye ameachwa ni Charles Ilanfya ambaye sio chaguo la Sven licha ya uongozi kuweka wazi kwamba usajili wa mchezaji huyo kutoka Klabu ya KMC ilikuwa ni pendekezo la kocha huyo.




Simba imewafuata FC Platinum ikiwa na orodha ya wachezaji 24 ambapo wanatarajiwa kucheza FC Platinum Desemba 23, mchezo wa kwanza kisha ule wa marudiano itakuwa ni kati ya Januari 5-6, Uwanja wa Mkapa.




Nafasi ya Morrison imechukuliwa na kiungo mpya Taddeo Lwanga ambaye ni ingizo jipya akiwa amesaini dili la miaka miwili.

KIKOSI CHA SIMBA KILICHOKWEA PIPA LEO KUWAFUATA WAZIMBABWE

 


KIKOSI cha Simba ambacho kimekwea pipa leo Desemba 18 kuifuata FC Platinum ya Zimbabwe. 


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Desemba 23 nchini Zimbabwe ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza

NYONI: SIMBA ITAIFUNGA FC PLATINUM






KIRAKA wa Klabu ya Simba, Erasto Nyoni amefunguka kuwa anaamini timu hiyo itaibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa ugenini dhidi ya Klabu ya FC Platinum unaotarajiwa kupigwa Desemba 23, Harare, Zimbabwe.



Simba tayari imewasili Jijini Harare leo Desemba 18 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo wa raundi ya kwanza ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Simba imefuzu hatua hiyo baada ya kuwaondosha Klabu ya Plateau United ya Nigeria kwenye mchezo wa raundi ya awali.

Akizungumza kuhusu mchezo huo Nyoni amesema: "Tunatumaini utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa wapinzani ambao tunakwenda kukutana nao.

"Lakini Wanasimba wanapaswa kutuamini na kuendelea kutuombea kwani tunaenda kwenye mapambano na naamini tunakwenda kushinda mchezo huu,".

SIMBA WATUA KIBABE ZIMBABWE,SERIKALI YAWAPOKEA, MPANDA MPIRA AKOSEKANA




WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Klabu ya Simba, leo Desemba 18 wamewasili salama nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa hataua ya kwanza dhidi ya FC Platinum.






Kikiwa chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck na kocha msaidizi Seleman Matola kimepata bahati ya kuonana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Profesa Emmanuel Mbennah.




Balozi huyo alipata nafasi ya kupiga picha ya pamoja na viongozi, wachezaji na benchi la ufundi baada ya chakula cha mchana.

Pia amepata nafasi ya kuongea na wachezaji wa timu ya Simba ambao wana kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.




Kikiwa kimeongozana na wachezaji 24 wanaoongozwa na nahodha John Bocco pamoja na Mohamed Hussein, 'Tshabalala' atakosekana mpanda mpira Bernard Morrison na Charlse Ilanfya ambao hawapo kwenye mpango wa Sven.

Simba SC yaisogelea Yanga juu



Simba imeendeleza moto wa kula viporo vyake baada ya jana kuwachapa wenyeji wao Mbeya City kwa bao 1-0, shukrani kwa kazi ya kiume ya mshambuliaji John Bocco aliyeitoa kibabe timu yake.

Hata hivyo haikuwa rahisi kwa Simba kupata ushindi huo baada ya wenyeji kuonyesha tofauti kubwa wakicheza soka la pasi na kasi lakini shida yao ikaja katika kumalizia wakikutana na ukuta mgumu wa wekundu hao chini ya mkongwe Joash Onyango na Ibrahim Ame ambaye jana alipata nafasi nyingine ya kuanza katika kikosi cha kwanza.

Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kufanya shambulizi kali dakika ya 20 na krosi ya Clatous Chama almanusura iitangulize timu yake, Bocco akishindwa kuunganisha na mpira kugonga mwamba na kipa Lameck Kanyonga kuuwahi.

Muda mrefu wa mchezo huo timu zote zilionekana kushindana kwa soka la katikati ya kiwanja wakishindwa kufika vyema katika kumalizia kufunga.


Ukuta wa Simba ulilazimika kufanya kazi ya ziada kupambana na mshambuliaji mwenye wa na Onyango.ADVERTISEMENT


Bocco dakika ya 33 akabadili ubao wa mabao akifunga bao safi la ufundi akipokea mpira kwa mguu wa kushoto kisha kumtoka kwa akili beki Juma Shemvuni na kufunga kwa shuti la ufundi akitumia mguu wa kulia akipokea pasi ya Chama.

Bao hilo lilikuwa ni la nane kwa msimu huu kwa Bocco akiendelea kufufua matumaini ya kuchukua tena kiatu cha ufungaji bora msimu huu huku bao hilo pia likiwa la 32 kwa timu yake.

Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha wenyeji na kuanza kujipanga tena kwa utulivu ambapo dakika 35 Seleman Ibrahim almanusura afunge bao kwa kichwa akipokea krosi kali ya Mpoki Mwakinyuke iliyowapita mabeki wa Simba na kukutana nayo nyuma yao.

Simba waliendelea kuliandama lango la Mbeya City ambapo dakika ya 37, Keneth Kunambi alifanya kazi nzuri kumbana Bocco aliyekuwa anasubiri kupiga bao la pili akiokoa krosi nzuri ya beki wa kulia Shomari Kapombe.

Simba ilipata nafasi nzuri katika kumaliza dakika 45 za kwanza lakini Meddie Kagere alishindwa kumalizia kwa kishwa krosi ya Hassan Dilunga.

Bao hilo lilidumu hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika kwa Simba kutoka kifua mbele dhidi ya Mbeya City katika Uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya.

Kipindi cha pili Simba waliingia kwa mabadiliko wakimtoa Bocco nafasi yake ikichukuliwa Chriss Mugalu akirejea baada ya kukaa nje kwa muda mrefu akiwa majeruhi.

Licha ya kuwa na mabadiliko hayo katika kikosi cha mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu, hakukuwa na mabadiliko yoyote kwa upande wa mabao.

Wekundu wa Msimbazi sasa wamefikisha pointi 29, wakiishusha Azam FC katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.




Mkutano mdogo Simba waja

Kamati ya Uchaguzi ya Simba imesisitiza kuwa, rais mpya wa klabu hiyo atakayechaguliwa kwenye uchaguzi mdogo atakuwa chaguo la wana Simba na si vinginevyo.


Simba itafaya uchaguzi mdogo Februari 7 ili kuziba nafasi ya mwenyekiti, Swedi Mkwabi aliyejiuzulu mwaka jana.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huo, Boniface Lihamwike alisema hakutokuwa na mchezo katika mchakato huo, akisisitiza kuwa utakuwa huru na wa haki.

“Atakayechaguliwa atachaguliwa kwa haki na wanachama wa Simba watampata kiongozi chaguo lao,” alisisitiza.

Moja ya sifa kubwa za mgombea wa nafasi hiyo, mbali ya kuwa Mtanzania, pia anapaswa kuwa mwanachama wa Simba kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu na mwenye elimu ya shahada ya kwanza inayotambuliwa na TCU na kila mgombea atalipia Sh300,000 ya fomu zinazoanza kutolewa leo hadi Desemba 24

Desemba 27 na 28 ni usaili, kutakuwa na siku nne za mapingamizi kuanzia Desemba 29 na Januari 5 hadi Februari 6 kitakuwa ni kipindi cha kampeni kwa wagombea wote waliopitishwa.

Alisema uchaguzi huo utaendeshwa chini ya kanuni za uchaguzi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuwa katiba ya Simba inawaruhusu kufanya hivyo kwa kuwa klabu hiyo haina kanuni za uchaguzi.

Simba ni Chama, Bocco tu






Kasi ambayo Yanga inaenda nayo kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu ni kama inawavuruga mabingwa watetezi wa ligi hiyo Simba, ambao juzi walipata ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City.

Licha ya Mbeya City kuwa ya tatu kutoka chini ya misamo wa ligi, iliibana Simba katika mchezo huo na kama ingeongeza kasi kidogo mchezo ungemalizika kwa sare.


Simba inacheza mechi zake katika presha ya kutetea ubingwa wao na kusaka taji la nne mfululizo la ubingwa msimu huu, huku kasi ya wapinzani wao wakubwa, Yanga ambayo imeanza kufunga idadi kubwa ya mabao katika mechi zake ikizidi kuwachanganya.

Miamba hiyo imezidiwa na Yanga pointi nane, huku pia ikiwa na mechi mbili mkononi za viporo dhidi ya KMC wanayocheza nayo Jumatano na dhidi ya Dodoma Jiji ugenini.

Ukiondoa mechi hizo, Simba ina mechi nne, mbili za kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi dhidi ya Namungo iliyopangwa kufanyika Jumapili na dhidi ya Azam itakayofanyika Desemba 27, wakati watani zao, Yanga wakiwa na michezo miwili dhidi ya Dodoma Jiji (Desemba 19) na itamaliza mzunguko wa kwanza kwa kucheza na Ihefu ugenini Desemba 26

SIMBA KAZINI LEO KUSAKA POINTI TATU MUHIMU DHIDI YA KMC




BAADA ya kumaliza kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine Mbeya kwa kushinda bao 1-0 Leo ina kazi ya kusaka pointi nyingine mbele ya KMC.






Tayari kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kimeshatia timu Dar es Salaam, jana Desemba 14 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara.




Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kuwa na mwendo mzuri ndani ya uwanja zikiwa kwenye viwanja vya Dar.

KMC imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro itaingia ndani ya uwanja ikiwa na hasira za kulipa kisasi cha kupoteza.




Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na wanahitaji pointi tatu muhimu.




Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anaamini utakuwa mchezo mgumu ila anahitaji pointi tatu muhimu.

Popular Posts