Mvua kubwa inayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam imesababisha mchezo wa kirafiki kati yetu dhidi ya Ndanda FC uliopangwa kufanyika leo jioni kwenye uwanja wa Azam Complex kuahirishwa.
Maandalizi ya mchezo yalikuwa yamekamilika kwa kiasi kikubwa lakini mvua inayoendelea imesababisha kuahirishwa.
Tangu asubuhi mvua imeendelea kunyesha na kusababisha miundo mbinu hasa barabara kutokuwa rafiki baada ya maji kuwa mengi hivyo tunajaribu kuepusha usufumbufu kwa mashabiki.
Uongozi wa klabu yetu unaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa mashabiki wetu ambao walikuwa nia ya kuja uwanjani kutupa sapoti.
Tunaangalia uwezekano wa mchezo huo kupigwa siku za mbeleni kama muda utapatikana.