Habari za Michezo kote Ulimwenguni

Powered by Blogger.

Mugalu atupia tena Simba ikiichapa Mlandege


Mshambuliaji wetu Chris Mugalu ameendelea kuwa rafiki wa nyavu baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 tuliopata dhidi ya Mlandege katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Oktoba 17.
Mugalu alitufungia bao la kwanza dakika ya saba kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Ibrahim Ajibu. Mlinzi wa kati Ibrahim Ame alitupatia bao la pili dakika ya 16 kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Luis Miquissone Baada ya mabao hayo tuliendelea kumiliki mpira huku tukitengeneza nafasi kadhaa za kufunga huku Mlandege wakifanya mashambulizi machache ya kushtukiza.
Kiungo Mzamiru Yassin akimthibiti mchezaji wa Mlandege wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam

Mugalu alipachika bao la tatu dakika ya 67 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Miquissone akiwa ndani ya 18 kabla ya kumpiga chenga mlinda mlango wa Mlandege. Dakika nne baadaye Mlandege walipata bao la kufutia machozi lililofungwa na Yahaya Kalua baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu. Kocha Sven Vandenbroeck aliwatoa Ame, Rally Bwalya na Miquissone nafasi zao zikachukuliwa na Herry Hussein, Seph Seleman na Andrew Michael.
Kikosi cha Simba kilichoanza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege

Popular Posts