Habari za Michezo kote Ulimwenguni

Powered by Blogger.

Wiki ya Machampioni: Simba yafanya usafi Daraja la Salender

Viongozi, wanachama na mashabiki wa Klabu ya Simba leo Jumamosi Agosti 15, wamefanya usafi katika fukwe za Bahari ya Hindi eneo la Daraja la Salender ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Machampioni. Zoezi hilo limedhaminiwa na Mo Extra na kuhudhuriwa na mgeni rasmi, Waziri wa Muungano na Mazingira, Mussa Azan Zungu.
Waziri Mussa Azan Zungu akishiriki usafi katika fukwe za Salender Bridge

Leo ni siku ua pili ya Wiki ya Machampioni kuelekea Simba Day Agosti 22 mwaka huu itakayofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo imeanza jana kwa kuzindua jezi na logo mpya ya klabu. Wiki ya Machampioni itaendelelea kesho kwa dua ya kuwaombea marehemu waliotangulia mbele ya haki ambao ni waasisi wa klabu. Kilele cha shughuli za Wiki ya Machampioni itakua Jumamosi ijayo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wafanyakazi, wanachama na mashabiki wa Simba wakishiriki usafi katika fukwe za Salender Bridge

Popular Posts