Klabu ya Simba imezindua logo mpya itakayoanza kutumika kuanzia leo ili kuendana na matakwa ya soko la kibiashara wakati timu ikiendeshwa kisasa.
Mwonekano katika logo hiyo ni jinsi ilivyokaa yaani mabadiliko kidogo lakini rangi nyekundu na nyeupe ambazo ndiyo nembo ya klabu zitaendelea kusalia kama zilivyo.
Mabadiliko haya yamefanyika kwa mujibu wa Katiba ya Simba Ibara ya 3: Bendera na Nembo ambayo inasema:
1). Simba Sports Club itatumia bendera yenye rangi nyekundu na nyeupe na nembo iliyopitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club Limited. Rangi nyingine inaweza kuongezwa kutokana na matakwa ya kibiashara.
Hii si jambo jipya kwa klabu kubadili logo hata klabu kubwa kama Barcelona, Juventus na Manchester United zimewahi kufanya hivyo.