Mlinzi wa kulia David Kameta 'Duchu' atavaa jezi nyekundu na nyeupe msimu ujao baada ya kujiunga na kikosi cha mabingwa wa nchi kutoka Lipuli FC kwa mkataba wa miaka mitatu.
Duchu ameonyesha uwezo mkubwa katika ligi iliyomalizika mwezi uliopita licha ya timu yake ya Lipuli kushuka daraja.
Duchu ni miongoni walinzi watatu wa kulia vijana waliofanya vizuri kwenye ligi msimu uliopita