Habari za Michezo kote Ulimwenguni

Powered by Blogger.

Simba yanasa straika wa Lusaka Dynamos

Mshambuliaji Chrispine Mugalu kutoka Lusaka Dynamos ya Zambia amejiunga  na klabu ya Simba tayari kwa msimu ujao wa 2020/21.

Mugalu, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, anakuwa mchezaji wa pili kutoka Ligi Kuu ya Zambia kujiunga na sisi baada ya kiungo tuliyemtangaza jana, Larry Bwalya, aliyetokea Power Dynamos.

Mpaka sasa tumekamilisha usajili wa wachezaji wanne wa kigeni ambao ni Mghana Bernard Morrison, Mkenya Joash Onyango, Mzambia Bwalya na Mugalu kutoka DRC.

Kwa upande wa wachezaji wa ndani ambao usajili wao tayari umeshakamilika ni David Kameta ‘Duchu’, Charles Ilamfia na Ibrahim Ame.

Popular Posts