Habari za Michezo kote Ulimwenguni

Powered by Blogger.

PICHA: Simba yaanza mazoezi rasmi leo

Kikosi chetu leo Jumatatu Agosti 17, kimeanza rasmi mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu 2020/21 itakayoanza Agosti 29, mwaka huu. Simba ilifanya mazoezi kuanzia saa 10 jioni katika Viwanja vya Mo Simba Arena, Bunju jijini Dar es Salaam ikiwa na wachezaji wote wakiwamo sita waliosajiliwa hivi karibuni chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck na wasaidizi wake. Wachezaji wageni ambao wameanza mazoezi kwa mara ya kwanza ni Joash Onyango, Chris Mugalu, Bernard Morrison, larry Bwalya,Ibrahim Ame, David Kameta na Charles Ilamfia.
Kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, akijadiliana jambo na msaidizi wake, Selemani Matola

Kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, akiwaongoza wachezaji wake katika mazoezi ya kwanza ya timu hiyo yaliyofanyika leo uwanja wa Mo Simba Arena

Beki mpya wa Simba, Joash Onyango, akifanya mazoezi ya kwanza na timu hiyo yaliyofanyika leo uwanja wa Mo Simba Arena

Kutoka kushoto ni Larry Bwalya, Chris Mugalu, Jonas Mkude na Bernard Morrison wakifanya mazoezi leo uwanja wa Mo Simba Arena

Bernard Morrison akijifua katika mazoezi ya kwanza ya Simba yaliyofanyika leo uwanja wa Mo Simba Arena

Popular Posts