Habari za Michezo kote Ulimwenguni

Powered by Blogger.

Ilamfia ajipiga kitanzi Simba


 Mshambuliaji Charles Martin Ilamfia amekamilisha usajili wa kujiunga na timu ya Simbaa baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kutoka KMC.

Ilamfia amekuwa kwenye kiwango bora katika msimu uliomalizika akiwa ndio mhimili kwenye safu ya ushambuliaji ya KMC hasa katika mzunguko wa pili wa ligi.

Nyota huyo mrefu mwenye mwili mkubwa amekuja kuongeza nguvu katika idara ya  ushambuliaji akisaidiana na nahodha John Bocco na Medie Kagere.

Usajili wa Ilamfia ndani ya Simba unatarajiwa kuwa mzuri na wenye mafanikio kutokana na uwezo wake pamoja na kujituma.

Popular Posts