Simba yapoteza mbele ya Prisons Sumbawanga
Kikosi chetu kimepoteza mchezo wa kwanza wa ligi msimu huu baada ya kukubali kipigo cha bao moja kutoka kwa Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.
Mchezo huo ulihusisha matumizi makubwa ya nguvu huku ufundi ukipungua hasa kwa upande wa Prisons.
Bao pekee kwenye mchezo huo lilifungwa na Samson Mbangula kwa kichwa dakika ya 49 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa kutoka upande wa kulia.
Kocha Sven Vandenbroeck aliwatoa Kapombe, Hassan Dilunga na Charles Ilanfya na kuwaingiza Kennedy Juma, Miraji Athuman na Mzamiru Yassin.
Katika mchezo huo, mlinzi wetu wa kulia Shomari Kapombe alishindwa kuendelea na mechi na kutolewa dakika ya 14 baada ya kupata majeraha.