Habari za Michezo kote Ulimwenguni

Powered by Blogger.

TANO BORA YA WAFUNGAJI BONGO









LIGI Kuu Bara msimu wa 2020/21 imezidi kuchanja mbunga huku vita kila seheu ikiwa ni ya moto kwa timu na mchezaji mmoja ndani ya timu.




Vita ya ufungaji nayo pia inazidi kupamba moto ambapo kwa msimu uliopita kiatu kilisepa na kuibukia Simba kwa mshambuliaji, Meddie Kagere ambaye alifunga jumla ya mabao 22.

Kwa msimu huu tayari Kagere ametupia mabao manne ndani ya Simba huku akizidi kupewa nafasi ya kufanya vizuri licha ya kukwama kuona nyavu kwenye mechi mbili za hivi karibuni.

Kwa sasa kinara wa utupiaji ni John Bocco ambaye amefunga jumla ya mabao 8, huyu pia ni nahodha wa Simba.

Adam Adam ni nyota anayekipiga ndani ya JKT Tanzania ametupia jumla ya mabao 7.

Prince Dube,staa wa Azam FC alianza kwa kasi kabla ya kupata majeraha ambayo yamemuweka nje ya uwanja ametupia jumla ya mabao 6.

Meshack Abraham ni mali ya Gwambina FC kibindoni ametupia jumla ya mabao 6.

Clatous Chama kiungo nyota wa Simba yeye ametupia jumla mabao 6.

KIPA SIMBA AIBUKIA IHEFU FC




DEOGRATIUS Munish maarufu kama Dida sasa atakuwa ni mali ya Ihefu FC inayoshiriki Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.






Kipa huyo ambaye amewahi kuitumikia Klabu ya Simba msimu wa 2018/19 na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara aliwahi pia kuwa kipa namba moja ndani ya Klabu ya Yanga.




Baada ya kuachwa na Simba alitumika ndani ya Klabu ya Lipuli FC ambayo kwa sasa imeshuka Ligi Kuu Bara na inapambana kurejea ndani ya ligi ikiwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.




Habari zinaeleza kuwa Dida anaibuka ndani ya Ihefu FC kuongeza nguvu kwenye lango kutokana na timu hiyo kuwa kwenye mwendo wa kusuasua.




Ikiwa imecheza jumla ya mechi 15 imefungwa jumla ya mabao 18 na imefunga mabao 6.




Kocha Mkuu wa Ihefu FC, Zuber Katwila amesema kuwa kwenye dirisha dogo wanahitaji kusajili wachezaji wenye uzoefu ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho.

MANARA AFUNGA NDOA, APEWA WOSIA NA KIKWETE




OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, usiku wa kuamkia leo Desemba 10, amefunga ndoa na mkewe Naheeda, katika msikiti wa Masjid Maamur.

Ndoa yake imehudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete, Shehe Mkuu wa mkoa wa Dar, Alhad Mussa Salum na watu wengine wengi maarufu.

Kikwete amesema kuwa Haji alimfuata nyumbani na kumshirikisha jambo hilo kwa ajili ya ndoa na akamuahidi kuja.

Kikwete amesema:"Hakuna ufundi kwenye ndoa kikubwa ni kustahimiliana na kuvumiliana kwa kuwa hakuna ufundi katika ndoa.

"Mnapaswa kuwa makini na kuskilizana katika ndoa, pia nakushauri ujue kwamba uwe na uvumilivu na kuona namna gani mnaweza kuleta watoto kwa kuulizana na kujua mambo yatakuaje.

"Baraka za Mungu kwa watoto ni zake ka kadri atakavyoamua, yale makundi yaache kwa kuwa kila mmoja anajua anachokipenda.




"Nilikuwa ninazungumza na mzee hapo nyuma akaniambia kwamba anahitaji wajukuu hivyo ni jambo la kheri na linahitaji subira kikubwa ninawapongeza katika hilo na ninaamini kwamba itakuwa kheri," amesema.

SVEN VANDENBROEC ATAJA SABABU YA KUMUACHA BONGO MORRISON

 



KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa nyota wao ambao wamebaki Bongo ni mpango na mbinu ya kiufundi kwa ajili ya mechi zijazo.
Miongoni mwa nyota ambao watakosekana kwenye mchezo wa leo ni Bernard Morrison mwenye bao moja na pasi mbili kiungo mshambuliaji wa Simba atakosekana kwenye mchezo wa Leo Desemba 13 dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Uwanja wa Sokoine majira ya saa 10:00 jioni.
Morrison hakusafiri na timu ambayo ilikwea pipa Desemba 11 kuwafuata wapinzani wake ambao watakutana leo Uwanja wa Sokoine.
Mbali na Morrison nyota wengine ni Ibrahim Ajibu mwenye bao moja na pasi mbili za mabao Charles Ilanfya, Kenedy Juma ambao wamepewa program na Sven Vandenbroeck huku Larry Bwalya mwenye pasi moja ya bao yeye ana matatizo ya kifamilia.


Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa sababu ya kuwakosa nyota hao ni kutokana na mpangilio wa ratiba ili wawe bora zaidi.

"Kuna wakati inabidi umpumzishe mchezaji ili awe bora kwenye mechi ijayo au kama sehemu ya mpango wa mbinu na ufundi,".

SIMBA WATANGAZA MCHAKATO WA UCHAGUZI WA MWENYEKITI

 


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara Klabu ya Simba, leo imetangaza mchakato mzima wa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya mwenyekiti utakaoanza leo Desemba 13, na kutarajiwa kukamilika Februari 7, mwakani,

Nafasi hiyo kwa sasa anaikaimu, Mwina Seif Kaduguda baada ya kuachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Swedi Mkwabi aliyejiuzulu wadhifa huo Septemba 14, mwaka jana baada ya kuhudumu kwa takribani miezi kumi pekee.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ndani ya klabu hiyo, Boniface Lihamwike amesema: "Tunataka kuwahakikishia Wanasimba na wadau wote wa michezo kiujumla kuwa uchaguzi huu utakuwa huru na wa haki.

Akitoa ratiba ya mchakato huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Steven Ally amesema: "Mchakato wa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba umeanza rasmi leo baada ya taarifa hii, na utaendelea mpaka Februari 7, 2021 ambapo ndiyo tunatarajia kufanya uchaguzi na kutangaza mshindi wa nafasi hiyo.

"Kwa taarifa zaidi kuhusu mchakato mzima tumebandika ratiba hii makao makuu ya klabu lakini pia watu wanaweza kuipata kupitia mitandao yetu ya kijamii, vigezo vya kuchukua fomu ni vile ambavyo vimewekwa bayana na Ibara ya 27 ya katiba ya klabu na pia vinapatikana kwenye fomu.

"Lakini kwa uchache ni lazima mgombea awe na elimu ya angalau Shahada inayotambuliwa na tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU), na kadi ya mwanachama hai kwa miaka mitatu huku gharama kwa fomu ikiwa ni Shilingi laki tatu," .

SIMBA YALIA NA WAAMUZI BONGO

 


LICHA ya Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 jana Desemba 13 na kusepa na pointi tatu mazima mbele ya Mbeya City, uongozi umeshusha lawma kwa waamuzi.

Bao la ushindi kwa Simba lilipatikana kipindi cha Kwanza kupitia kwa nahodha John Bocco aliyepachika bao hilo kwa pasi ya Clatous Chama. 

Mwamuzi wa kati jana alikuwa ni Martin Sanya alijitahidi kwenda na presha ya mchezo wa jana kutokana na timu zote kuwa na uhitaji wa pointi tatu. 


Mbeya City malengo yao makubwa ni kujinasua kwenye mstari wa kushuka daraja na Simba wao jambo lao ni kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara. 


Mtendaji Mkuu wa Simba, (CEO), Barbara Gonzalez amesema kuwa bado maamuzi ya waamuzi ni tatizo ndani ya Ligi Kuu Bara. 


Ushindi wa Simba jana unaipandisha kutoka nafasi ya tatu mpaka nafasi ya pili ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza mechi 13.


Yanga ni vinara wakiwa na pointi 37 baada ya kucheza mechi 15 na nafasi ya tatu ni Azam FC wenye pointi 27 baada ya kucheza mechi 14.


Mbeya City ipo nafasi ya 16 baada ya kucheza mechi 15 na ina pointi 12 kibindoni. 

BEKI SIMBA ATAJWA NDANI YA COASTAL UNION

 



IMEELEZWA kuwa beki wa kati wa Yusuph Mlipili ameingia anga za Coastal Union inayonolewa na Kocha Mkuu,  Juma Mgunda. 


Mlipili ambaye aliachwa na Simba msimu uliopita kutokana na kukosa nafasi kikosi cha Kwanza ni miongoni mwa wazawa mwenye uwezo mkubwa akiwa ndani ya uwanja.


Ujio wa Joash Onyango na Pascal Wawa ambao ni mabeki wa kati uliongeza ufinyu wa namba kikosi cha Kwanza jambo lililofanya nyota huyo apigwa chini mazima licha ya uwezo wake.


 Mgunda ameweka wazi kwamba moja ya sehemu ambayo ataifanyia maboresho ni sehemu ya beki kwa kuwa baada ya kuondoka kwa pacha ya Bakari Mwamnyeto anayekipiga Yanga na Ibrahim Ame ndani ya Simba mambo yamekuwa magumu.


Kwa msimu wa 2020/21 inashikilia rekodi ya kufungwa mabao mengi ambayo ni 7-0 ilifungwa na Simba, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.


Mgunda amesema:"Ni lazima nifanyie maboresho safu yangu ya ulinzi na ushambuliaji Kwenye dirisha dogo hivyo mipango ikikamilika kila kitu kitawekwa wazi,".

Popular Posts